Tazama maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa umeme Alhamisi

Baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Machakos, Busia,Kajiado, Meru, Kilifi, Mombasa na Tana River.

•Sehemu kadhaa za maeneo ya Westlands na Upperhill yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 8.

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Machakos, Busia,Kajiado, Meru, Kilifi, Mombasa na Tana River.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za maeneo ya Westlands na Upperhill yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Tala, Kangundo, na Machakos Eastleigh katika kaunti ya Machakos zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Mungatsi na Kwangamor katika kaunti ya Busia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kajiado, sehemu kadhaa za eneo la Korompoi zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni

Sehemu kadhaa za maeneo ua Urru na Miathene katika kaunti ya Meru pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za eneo la Watamu katika kaunti ya Kilifi zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Katika kaunti ya Mombasa, sehemu za eneo la Miritini zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Hola na Bura katika kaunti ya Tana River pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.