Tazama maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa stima Jumatatu

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Februari 12.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita yatakosa umeme kati ya saa mbili  asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Kiambu, Kilifi, Homa Bay, Embu na Nyeri

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Februari 12.

Katika taarifa ya siku ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Kiambu, Kilifi, Homa Bay, Embu na Nyeri.

Katika kaunti ya Machakos, sehemu za barabara ya Kitui zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Kasufini na Mkoamoto katika kaunti ya Kilifi pia yatakosa umeme.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Thogoto na PCEA University katika kaunti ya Kiambu yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Homa Bay, sehemu kadhaa za maeneo ya mji wa Oyugis  yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa jioni.

Umeme pia utakatizwa katika baadhi ya sehemu za Kavutiri na Kianjokoma katika kaunti ya Embu kwanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za soko la Chaka, Mbiriri na Nyaribo katika kaunti ya Nyeri pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.