KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakuwa bila stima leo, Alhamisi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 22.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Elgeyo Marakwet, Nyeri, Mombasa, Kilifi na Taita Taveta.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 22.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Elgeyo Marakwet, Nyeri, Mombasa, Kilifi na Taita Taveta.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Gigiri na Muthaiga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kapsowar katika kaunti ya Elgeyo Marakwet zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Tetu, Kigogoini na Wandumbi katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za Port Reitz na Migadini katika kaunti ya Mombasa pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Katika kaunti ya Kilifi, sehemu kadhaa za maeneo ya Kikambala, Mavueni, Chasimba zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Maisenyi katika kaunti ya Taita Taveta zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.