Mwanahabari mkongwe Rita Tinina amefariki dunia. Polisi walisema mwili wa Tinina ulipatikana katika nyumba yake ya Kileleshwa jijini Nairobi Jumapili, Machi 17.
Alipaswa kuwa zamu katika NTV ambako alifanya kazi lakini alishindwa kuripoti.
Hilo lilifanya wasimamizi wa kazi yake waende kwenye nyumba ambayo mwili huo ulipatikana.
Chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana, polisi walisema. Familia yake ilikuwepo polisi walipofika kuuchukua mwili huo hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Alikuwa ni mama wa msichana mmoja.