Gavana Sakaja na waziri Nakhumicha hawafai kutilia shaka mgomo wa madaktari-KMPDU

"Gavana Sakaja na Waziri hawafai kutilia shaka mgomo wetu. Tulitia saini mkataba nao," Atellah alidai.

Muhtasari
  • "Saa hii mimi nimefanya kazi ya afya sasa wameanza kunionea wivu wanaleta nyenyenye...cartels ndio wanasponsor maandamano,"
Madaktari wanaofunzwa kazini wakiongozwa na katibu mkuu wa Muungano wa Madaktari Daktari Davji Atellah na Naibu katibu mkuu Daktari Miskellah Dennis wakati wa mkutano na wanahabari jijini Nairobi Mei 9, 2023.
Madaktari wanaofunzwa kazini wakiongozwa na katibu mkuu wa Muungano wa Madaktari Daktari Davji Atellah na Naibu katibu mkuu Daktari Miskellah Dennis wakati wa mkutano na wanahabari jijini Nairobi Mei 9, 2023.
Image: STAR

Katibu mkuu wa Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya Davji Atellah amewaambia Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja na Waziri wa Afya Susan Nakhumicha kutotilia shaka uamuzi wa madaktari kugoma.

"Gavana Sakaja na Waziri hawafai kutilia shaka mgomo wetu. Tulitia saini mkataba nao," Atellah alidai.

Alisema Katiba pia ilieleza kuwa kila mfanyakazi ana haki ya kufanya maandamano ya amani, akibainisha kuwa haogopi vitisho vinavyotolewa kwao.

"Si mara ya kwanza tunapata vitisho. Ni wimbi la kupita," Atellah alipokuwa kwenye mahojiano na runinga ya Citizen.

Sakaja wiki jana alitoa makataa kwa madaktari walio na uhusiano na Nairobi ambao walikuwa wakishiriki mgomo unaoendelea nchini kote wa madaktari kurejea kazini mara moja.

Aliwapa madaktari jijini Nairobi saa 12 kurejea kazini, akisisitiza kuwa hataruhusu maisha ya wagonjwa kusalia hatarini kutokana na masuala anayosema yanaweza kutatuliwa hatua kwa hatua.

“Nimewapa madaktari wa Nairobi saa 12 kujitokeza katika hospitali zetu. Wale wanaotaka kuendelea kufanya kazi katika kaunti ya Nairobi, mna saa 12 za kujitokeza katika hospitali zetu kwa sababu jukumu nililonalo ni kuhakikisha kuwa ninatoa huduma za afya kwa wakazi wa Nairobi,” Sakaja alisema.

Sakaja alisema kuwa masuala kuhusu kushindwa kwa serikali ya kitaifa kuwachapisha wahudumu wa afya na kutofuatwa kwa Makubaliano ya Pamoja ya Madaktari 2017 hayahusiani moja kwa moja na mamlaka ya kaunti hivyo madaktari walioajiriwa kaunti ya Nairobi wanapaswa kurejea kazini.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya Susan Nakhumicha alishutumu makampuni ya serikali kwa kufadhili mgomo unaoendelea wa madaktari ambao uliingia siku ya 10 nchini kote Jumamosi.

"Saa hii mimi nimefanya kazi ya afya sasa wameanza kunionea wivu wanaleta nyenyenye...cartels ndio wanasponsor maandamano,"