Kaunti 13 kukumbwa na kukatizwa kwa umeme Jumanne- KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 24.

Muhtasari

•KPLC imetangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti kumi na tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Nairobi, Uasin Gishu, Trans Nzoia, Bungoma, Busia, Homa Bay, Migori, Nyamira, Kisii, Nyeri, Kirinyaga, Kiambu, na Kwale.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 24.

Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti kumi na tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Uasin Gishu, Trans Nzoia, Bungoma, Busia, Homa Bay, Migori, Nyamira, Kisii, Nyeri, Kirinyaga, Kiambu, na Kwale.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za barabara ya Ngong, Kibera na Brookside Drive zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Ngecheck na Ngeria katika kaunti ya Uasin Gishu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chepchoina, Kimondo na Suam katika kaunti ya Trans Nzoia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Bungoma, eneo la Matisi Water Treatment Plant litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Eneo la Nesewa Health Centre katika kaunti ya Busia pia litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo kadhaa ya kaunti ya Homa Bay yakiwemo Ndiwa,Kalamindi na Wachara yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Katika kaunti ya Migori, sehemu kadhaa za maeneo ya Rongo, Kanyawanga na Kokuro zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Ikonge, Ekerenyo, na Nyaramba katika kaunti ya Nyamira zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu za kaunti ya Kisii zikiwemo hospitali ya Nyangena na Nyabururu zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa saba mchana.

Maeneo ya Kanjama, Ndira na Umbui katika kaunti ya Nyeri pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kirinyaga, maeneo ya Mutitu, Mukinduri na Kaharo yatashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kibubuti,Komo, Githima, na Magana  katika kaunti ya Kiambu pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Msambweni katika kaunti ya Kwale zitashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.