Maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme Jumatano- KPLC

Baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Aprili 3. 

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nyeri, Bomet, Uasin Gishu, Kisii, na Embu.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Aprili 3.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nyeri, Bomet, Uasin Gishu, Kisii, na Embu.

Katika kaunti ya Nairobi, mtaa wa Garden Estate utaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Muruguru, Githiru, Marua, Gacharageini, Kagongo, Mioro, Kiawarigi na Gitunduti katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Mulot na Longisa katika kaunti ya Bomet pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za mji wa Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Kisii, baadhi ya sehemu za maeneo ya Menyinkwa na Nyachenge zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa saba mchana.

Baadhi ya sehemu za Siakago Ex Kyeni katika kaunti ya Embu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.