Shirika la Reli la Kenya (KRC) Larejesha Huduma ya Treni kwa Wasafiri

Huduma katika Kijiji cha Embakasi, Lukenya, SGR Link na njia za Syokimau zitarejelewa kuanzia kuanzia leo Jumanne.

Muhtasari

•Njia za Limuru na Ruiru zitaendelea kusimamishwa kutokana na ukarabati.

• Huduma katika Kijiji cha Embakasi, Lukenya, SGR Link na njia za Syokimau zitarejelewa  kuanzia kuanzia leo Jumanne

Mamlaka ya Reli ya Kenya
Mamlaka ya Reli ya Kenya
Image: picha:twitter /Hisani

Shirika la Reli la Kenya (KRC) limetangaza kurejeshwa kwa baadhi ya huduma za treni ya abiria baada ya kusimamishwa kutokana na mvua kubwa inayonyesha.

KRC mnamo Aprili 24 ilisimamisha treni ya abiria ambayo husafirisha wasafiri kwenda na kutoka katikati mwa jiji la Nairobi kila siku katika njia tano; Embakasi, SGR Link na Syokimau, Limuru, Lukenya na Ruiru

Siku ya Jumatatu, Shirika la Reli la Kenya lilisema katika taarifa kwa umma kuwa litarejelea huduma katika Kijiji cha Embakasi, Lukenya, SGR Link na njia za Syokimau kuanzia leo Jumanne.

Hata hivyo, njia za Limuru na Ruiru zitaendelea kusimamishwa kutokana na ukarabati unaoendelea kwenye njia za reli, ilisema.

"Pia tungependa kushauri umma kwamba huduma za treni za abiria zinaweza kubadilika, kulingana na hali ya hewa na masuala mengine ya usalama. Tunashukuru kwa subira  tunapojitahidi kurejesha hali ya kawaida,” ilisema taarifa ya umma kutoka kwa usimamizi wa KRC.