Wakaazi wa Nairobi waonywa kuhusu mvua kubwa leo

Mvua ya wastani hadi kubwa inatarajiwa kuanzia alasiri, jioni na usiku kulingana na ramani ya muda wa saa 3 ya Nairobi.

Muhtasari

•Mvua ya wastani hadi kubwa inatarajiwa kuanzia alasiri, jioni na usiku kulingana na ramani ya  muda wa saa 3 ya Nairobi.

• Fahamu hali ya hewa na uwe tayari!

Mvua kubwa inakuja
Image: HISANI

Wakazi wa Nairobi wameonywa kuhusu mvua  kubwa hivi leo na wametakiwa kuchukuwa tahadhari za kiusalama.

Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya imewaonya wakazi wa Nairobi kujiandaa kwa ajili ya mvua za wastani hadi kubwa zinazotarajiwa Jumanne, Mei 7, 2024.

Kulingana na idara ya hali ya hewa, mvua hiyo inatarajiwa kunyesha kuanzia alasiri hadi jioni na  usiku wa leo.

"Mvua ya wastani hadi kubwa inatarajiwa kuanzia alasiri, jioni na usiku kulingana na ramani ya  muda wa saa 3 ya Nairobi. Fahamu hali ya hewa na uwe tayari!" mtaalam wa hali ya hewa alisema katika taarifa ya   hivi karibuni.

Mnamo Jumatatu, ripoti ya hali ya hewa ilionyesha kuwa mvua itaendelea katika sehemu kubwa za nchi kwa siku saba zijazo.

Hasa, mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika maeneo kama vile Nyanda za Juu za Kati, Magharibi mwa Kenya, na Bonde la Ufa katika nusu ya kwanza ya kipindi hiki.