Gachagua ahudhuria ibada ya kumbukumbu ya wahanga wa mafuriko ya Mai Mahiu

Mkasa wa Mai Mahiu ulisababisha vifo vya watu 60, huku watu 51 wakiwa bado hawajulikani waliko na wengine 52 kupata majeraha wakati wa matukio yaliyotokea wiki iliyopita.

Muhtasari

• Mbunge wa Naivasha Jane Kihara alipongeza serikali kwa hatua yake ya haraka ya kuzuia visa zaidi.

• Aliwataka wakazi kuwa waangalifu wakati huu wa mvua.

DP Gachagua ahudhuria ibada ya wafu Mai Mahiu
DP Gachagua ahudhuria ibada ya wafu Mai Mahiu
Image: DPCS

Naibu Rais Rigathi Gachagua amehudhuria ibada ya kuwakumbuka wahanga wa mafuriko ya Mai Mahiu.

Hafla hiyo inafanyika katika Viwanja vya Mo Gas huko Mai Mahiu, Nakuru.

Gavana wa Nakuru Susan Kihika aliandamana na Gachagua.

Viongozi wengine ni Ann Wamuratha (Kiambu), Martha Wangari (Gilgil), Mburu Kahangara (Lari), George Koimburi (Juja) na Simon King'ara (Ruiru).

Wengine ni pamoja na Kamande Mwafrika (Roysambu), Jane Kihara (Naivasha), na Mary Wa Maua (Maragua) miongoni mwa wengine.

Mkasa wa Mai Mahiu ulisababisha vifo vya watu 60, huku watu 51 wakiwa bado hawajulikani waliko na wengine 52 kupata majeraha wakati wa matukio yaliyotokea wiki iliyopita.

Mbunge wa Naivasha Jane Kihara alipongeza serikali kwa hatua yake ya haraka ya kuzuia visa zaidi.

Aliwataka wakazi kuwa waangalifu wakati huu wa mvua.

"Tuna furaha kuwa na naibu rais hapa kutufariji na tuna furaha," Kihara alisema.