Dereva wa Probox akamatwa kwa kubeba wanafunzi 13 Kitale

Kulingana na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama, gari hilo lilizuiliwa kwa kubeba wanafunzi 13.

Muhtasari
  • Katika picha zilizoshirikiwa na NTSA, wanafunzi hao walionekana wakiwa wamerundikana kwenye gari.
Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

olisi wamemkamata dereva wa probox aliyepatikana akiwa amebeba abiria kupita kiasi kwenye barabara ya Kitale - Kapenguria.

Kulingana na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama, gari hilo lilizuiliwa kwa kubeba wanafunzi 13.

Katika picha zilizoshirikiwa na NTSA, wanafunzi hao walionekana wakiwa wamerundikana kwenye gari.

Wengine walionekana wakiwa wamekaa kwenye buti la gari hadi halikuweza kufunga.

Waliokaa mbele walibebana.

NTSA ilisema dereva huyo alikamatwa na atashtakiwa kortini.

Mamlaka ilitoa wito kwa madereva wa magari kuwa waangalifu wanaposhughulikia watoto wa shule.

"Pamoja tuhakikishe watoto wetu wamefika shuleni salama," NTSA ilisema.

Haya yanajiri wakati NTSA imezindua ukaguzi wa kufuata sheria za usalama barabarani katika barabara kuu kote nchini.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama barabarani huku wanafunzi wakianza kuripoti shuleni Jumatatu.

Polisi na mamlaka ya usalama barabarani wamekamata magari kadhaa kwenye njia mbalimbali katika msako huo unaolenga kuhakikisha uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani.