Kenya Power: Kaunti tisa kukosa huduma za umeme leo

Nairobi ni moja kati ya kaunti ambazo zitakabiliwa na kukatizwa kwa umeme katika eneo ya Buruburu

Muhtasari

•Haya yanaripotiwa hili kuwezesha kutengenezwa kwa mtandao ya umeme katika maeneo yote yaliyoathirika na mvua kubwa ambayo ilisababisha uharibifu nchini.

Kenya Power
Image: HISANI

Kaunti tisa zitaathiriwa na kukatizwa kwa umeme leo (Jumanne, Mei 14), Kenya Power yatangaza kupitia mtandao wa X.

Haya yanaripotiwa hili kuwezesha kutengenezwa kwa mtandao ya umeme katika maeneo yote yaliyoathirika na mvua kubwa ambayo ilisababisha uharibifu nchini.

Katika Kaunti ya Nairobi, eneo kubwa la Buruburu umeme utakatizwa kuanzia saa tisa asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo mahususi ni pamoja na; Sehemu ya Kimathi Est, Jerusalem, Jericho, Metro Villas, Harambee Est, Uhuru Est, Sehemu ya Buru Ph1, Buruburu Pri & adjacent customers.

Kaunti zingine ni pamoja na Nandi county, Siaya, Tana river, Lamu, Uasin Gishu, Kilifi, Kisii na Nyeri.