Unda nafasi za kazi kabla ya kuongeza ushuru, balozi Meg Whitman amuambia Ruto

Watu wengi wanapokuwa na mapato ya kutosha wanaweza kulipa kodi

Muhtasari

•"Kuna njia mbili; kuongeza kodi na pia kupanua misingi ya kodi ambayo ni idadi ya watu wanaotozwa kodi na ndiyo maana ajira."

•Watu wengi wanapokuwa na mapato ya kutosha wanaweza kulipa kodi.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman. Picha: TWITTER
Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman. Picha: TWITTER

"Tengeneza Kazi Kwanza Kabla ya Kuongeza Kodi,' U.S. Balozi nchini Kenya Meg Whitman ameonekana kutoridhishwa na mpango wa Rais William Ruto wa kuongeza kiwango cha ushuru wa Kenya kutoka asilimia 14 hadi 22 kufikia mwisho wa muhula wake.

Akizungumza katika mahojiano siku ya  Jumatano, Whitman alisisitiza umuhimu wa kutoza ushuru katika kuimarisha mazingira tulivu ya kiuchumi nchini Kenya.

"Ushuru ni suala katika kila nchi na tunachosikia katika kampuni za Amerika ni kwamba Kenya inahitaji tu kutozwa ushuru wa chini lakini thabiti; kuweka ushuru sawa kwa miaka mitatu, minne, au mitano kwa sababu biashara hufanya uwekezaji wa faida, " alisema Balozi wa Marekani Whitman.

"Hutarajii kwamba utatengeneza pesa zako katika mwaka mmoja lakini miaka mitano, miaka sita, miaka saba; kwa hivyo uthabiti wa kodi ni muhimu."

Akizungumzia mbinu za kuongeza kodi, Whitman alitetea jia za kutengeneza kodi kupitia uundaji wa kazi badala ya kuongeza viwango vya ushuru.

"Kuna njia mbili; kuongeza kodi na pia kupanua misingi ya kodi ambayo ni idadi ya watu wanaotozwa kodi na ndiyo maana ajira ni muhimu sana kwanza. Kazi zinazolipa vizuri, na malipo ya kudumu na baadhi ya marupurupu.

"Watu wengi wanapokuwa na mapato ya kutosha wanaweza kulipa kodi kwa hivyo upanue idadi ya watu."

Mnamo Alhamisi Rais Ruto alitetea mpango wa serikali wa kutoza ushuru wa ziada kwa Wakenya, akisema kuwa ni sehemu ya mkakati mpana wa kuimarisha mapato ya nchi na kupunguza utegemezi wa kukopa.

Ruto pia alibainisha kuwa anakusudia kuongeza kiwango cha wastani cha kodi nchini kutoka asilimia 14 ya sasa hadi asilimia 16 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na kufikia kiwango cha kati ya asilimia 20 na 22 ifikapo mwisho wa muda wake wa uongozi.

Huku akikubali mzigo wa kiuchumi ambao Wakenya watalazimika kubeba ili kufikia lengo hilo, Ruto alisisitiza kuwa manufaa ya muda mrefu yatahalalisha ongezeko la ushuru.

"Dhamira yangu ni kusukuma Kenya, ikiwezekana mwaka huu tutakuwa 16% kutoka 14%. Nataka katika kipindi changu, niiache kati ya 20 na 22%. Itakuwa ngumu,watu watalalamika lakini najua hatimaye watashukuru kwamba fedha tunazokwenda kukopa Benki ya Dunia ni akiba kutoka nchi nyingine,” alisema.