Mwanamke akamatwa kwa kumpiga mawe mume hadi kifo kwa mzozo wa Ksh.3,000 Makueni

Mwili wa mzee huyo ulipelekwa katika chumba cha maiti cha Tawa.

Muhtasari
  • Kulingana na Albanus Mutula, msaidizi wa chifu wa eneo hilo, wanandoa hao walitofautiana kuhusu Ksh.3,000 huku marehemu akimshutumu mkewe mchanga kwa kuiba pesa hizo.
Pingu
Image: polisi wawili washikwa kwa madai ya hongo

Polisi Mbooni Mashariki, Kaunti ya Makueni wanamshikilia mwanamke mwenye umri wa miaka 32 nayedaiwa kumuua mumewe mwenye umri wa miaka 82.

Kulingana na Albanus Mutula, msaidizi wa chifu wa eneo hilo, wanandoa hao walitofautiana kuhusu Ksh.3,000 huku marehemu akimshutumu mkewe mchanga kwa kuiba pesa hizo.

Syombua Musau anadaiwa kumpiga mumewe kwa mawe mgongoni na kumuua papo hapo.

Mwanamke huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mbumbuni akisubiri kusomewa mashitaka.

Mwili wa mzee huyo ulipelekwa katika chumba cha maiti cha Tawa.

Msimamizi huyo aliwataka wakazi kutafuta njia mwafaka za kutatua tofauti zao bila kuchukua hatua za kurudi nyuma.

uy67