KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakosa umeme leo, Jumatano

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Mei 29.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na  West Pokot, Kisumu, Migori, Nyamira, Nyeri, Laikipia, Kiambu, Kitui, na Mombasa.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Mei 29.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  West Pokot, Kisumu, Migori, Nyamira, Nyeri, Laikipia, Kiambu, Kitui, na Mombasa.

Katika kaunti ya West Pokot, eneo la Sirikwa Safaris litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Katolo na Ombeyi katika kaunti ya Kisumu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Sehemu kadhaa za mji wa Migori na Oruba katika kaunti ya Migori zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja asubuhi.

Katika kaunti ya Nyamira, sehemu kadhaa za maeneo ya Ikonge na Mabariri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kiawarigi na Gitunduti katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Gathiuru na Mirera katika kaunti ya Laikipia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kihunguro na Rainbow zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Waita na Kamuongo katika kaunti ya Kitui pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Nyali na Mkomani katika kaunti ya Mombasa pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.