DP Gachagua asema kushika mke mkono ni ‘mambo ya wazungu’

'Hivi karibuni,Rais atanituma Marekani na nitaenda na wewe,nakuhakikishia kukushika mkono tutakapotua Marekani,ila tukirudi Kenya tutaendelea na maisha yetu ya kawaida.'Gachagua alimhakikishia mkewe mama Dorcas

Muhtasari

•Naibu rais ametaja kushikana mkono kati ya Rais Ruto na mama Rachel ni mambo ya kiamerika hii ni baada ya mkewe mama Dorcas kumshinikiza aige rais ruto

•Gachagua aidha amemhakikishia mkewe Dorcas kumshika mkono watakapozuru Marekani ila wakirejea Kenya,waendelee na maisha yao ya kawaida.

DP Gachagua
DP Gachagua
Image: HISANI

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewachekesha baadhi ya wabunge waliohudhuria maombi  ya kitaifa kwa kufichua kuwa mkewe Dorcas alitaka kushikwa mkono hasa baada ya Rais Ruto na mama Rachel kushikana kule Marekani.

Gachagua alibainisha kuwa kitendo cha Rais William Ruto kumshika mkono mke wake Rachel Ruto wakati wa ziara yake ya kiserikali nchini Marekani kilimshawishi mkewe naibu rais, Dorcas ambaye alimtaka Gachagua kuiga vivyo hivyo. Kulingana na Gachagua,mkewe Dorcas  alitaka amshike mkono hata ndani ya nyumba.

Gachagua aliongeza kuwa wanaume wengi kote nchini walikabiliwa na changamoto hiyo kufuatia kitendo cha Ruto na Rachel cha kushikana mikono Marekani.

"Wakenya wote walikuwa wakifuatilia ulichokuwa unafanya Marekani. Kuna kitu ambacho ulikuwa ukifanya huko ambacho kilizua matatizo kwa waume wengi kote nchini..Ulipokuwa ukitembea huku umeshika mkono wa mama Rachel,ulitupa shinikizo kubwa. Wenzi wetu wakiongozwa na mgodi mchungaji mama Dorcas walikuwa wakidai tumwige Rais na kushika mkono wao popote tuendapo." Gachagua alisema.

Hata hivyo, Gachagua alifikia hitimisho kwamba kushikana mikono kwa Ruto ni jambo la kiamerika tu baada ya Ruto kumwacha Rachel  mara baada ya kukwea gari lake katika Hoteli ya Serena walipokuwa wanakuja kwa mkutano wa maombi ya kitaifa.

Hata hivyo,Gachagua alimhakikishia mkewe Dorcas kwamba atamshika mkono watakapozuru Marekani kwa ajili ya kazi yake.

"Mke wangu mchungaji Dorcas, yote hayajapotea.Hivi karibuni Rais atanituma  kwenda Marekani na nitakwenda nawe. Una uhakika wangu kwamba kwa muda huu tuko kwenye ardhi ya Amerika, nitakushika mikono hadi tuondoke nchini, lakini tukirudi, tafadhali turudi kwenye maisha yetu," Gachagua alimwambia mkewe mchungaji Dorcas.