Gavana wa Kwale Achani Kuongeza Ada kwa Muguka Kutoka Ksh 10K hadi Ksh 300K

Gavana Achani aliendelea kuwataka wakaazi sio tu kupiga vita unywaji wa Muguka bali pia dawa zingine kama vile bangi na aina zingine za dawa haramu.

Muhtasari
  • Achani pia alipuuzilia mbali madai ya hivi majuzi ya kuunga mkono uuzaji wa Muguka katika Pwani, akishikilia kuwa zao hilo lilisababisha madhara zaidi kuliko manufaa kwa wapiga kura wake.
Miraa
Image: maktaba

Kama sehemu ya hatua kali za kuzuia usambazaji na uuzaji wa Muguka katika Kaunti ya Kwale, Gavana Fatuma Achani Jumamosi alitangaza mipango ya kuongeza ushuru wa zao hilo kutoka Ksh10,000 hadi Ksh300,000 kwa lori.

Gavana alipokuwa akiwahutubia wakazi wakati wa sherehe za Siku ya Madaraka alibainisha kuwa ongezeko la ada litaanza kutekelezwa baada ya kuidhinishwa kwa Mswada wa Fedha wa Kaunti wa 2024/2025.

Kulingana na Achani, ongezeko la tozo hizo litahakikisha kuwa unywaji wa Muguka unadhibitiwa kwa kufanya zao hilo kutoweza kumudu wateja wengi.

“Tayari tumepitisha mswada wa Fedha na unasubiri idhini yangu ili uwe sheria. Yeyote atakayekuja na lori la Muguka atalazimika kulipa Ksh300,000,” gavana huyo alitangaza.

Achani pia alipuuzilia mbali madai ya hivi majuzi ya kuunga mkono uuzaji wa Muguka katika Pwani, akishikilia kuwa zao hilo lilisababisha madhara zaidi kuliko manufaa kwa wapiga kura wake.

"Tumeweka bei mpya ili kuhakikisha kwamba hata ikiwa mazao yanauzwa katika kaunti, mtu asiye na uwezo wa kifedha hataweza kuinunua," Achani alifichua.

Gavana huyo mkali alisema licha ya kaunti zingine za Pwani kupiga marufuku zao hilo aliamua kuidhinisha uuzaji wake kwa kuzingatia sheria.

Hata hivyo, usambazaji na uuzaji wake ungefuatiliwa na kudhibitiwa sana ili kuhakikisha hausababishi madhara kwa kizazi cha vijana.

Gavana Achani aliendelea kuwataka wakaazi sio tu kupiga vita unywaji wa Muguka bali pia dawa zingine kama vile bangi na aina zingine za dawa haramu.

Maoni ya Fatuma Achani yanakuja kinyume na madai ya hivi majuzi kwamba aliidhinisha uuzaji wa zao hilo lililozua utata katika kaunti hiyo.