KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo Jumatatu

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Juni 3.

Muhtasari

•KPLC imetangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri. 

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Bomet, Nandi, na Kisii.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Juni 3.

Katika taarifa ya siku ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri. 

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Bomet, Nandi, na Kisii.

Katika kaunti ya Bomet, baadhi ya sehemu za maeneo ya Silibwet, Merigi na Tenwek zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Chebarbar, Baraton University, na Kipchapo Factory katika kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Kisii, baadhi ya sehemu za maeneo ya Geteri, na Kanyimbo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tano asubuhi.