Polisi wawakamata washukiwa 2 wakiwa na bangi Kangemi

Polisi walisema kukamatwa kwa washukiwa hao wawili kulifuata kidokezo kutoka kwa umma.

Muhtasari
  • Polisi walisema kidokezo kutoka kwa umma kilionyesha kuwepo kwa shehena hiyo haramu kwenye sacco ya matatu waliyokuwa wakisafiria.
Image: DCI/ X

Washukiwa wawili wa kiume walikamatwa Jumatano asubuhi kwa madai ya ulanguzi wa mihadarati kwa kujifanya abiria kwenye gari.

Polisi walisema washukiwa hao wawili walitolewa kwenye matatu iliyokuwa inaelekea Nairobi kutoka Busia kwenye barabara ya juu ya Kangemi, na kutoka kwao, marobota 16 ya bangi yakiwa yamefichwa kwenye mabegi yao ya kusafiria yalikamatwa.

Polisi walisema kukamatwa kwa washukiwa hao wawili kulifuata kidokezo kutoka kwa umma.

Polisi walisema kidokezo kutoka kwa umma kilionyesha kuwepo kwa shehena hiyo haramu kwenye sacco ya matatu waliyokuwa wakisafiria.

Kulingana na ripoti za polisi, washukiwa hao wawili wamekabidhiwa kwa maafisa wa upelelezi wa Kupambana na Dawa za Kulevya walio katika makao makuu ya DCI kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi.

"Kukamatwa kwa wawili hao, Samuel Okello na Antony Omingo, kulifuatia kidokezo cha #FichuakwaDCI kutoka kwa umma, kilichoonyesha kuwepo kwa shehena hiyo haramu katika matatu ya Trippin Shuttle Sacco waliyokuwa wakisafiria.

Okello na Omingo wamekabidhiwa kwa maafisa wa upelelezi wa Kupambana na Dawa za Kulevya walio katika makao makuu ya DCI ili kufanyiwa kazi zaidi," Taarifa ya DCI ilisoma.