Serikali yajibu madai ya ofisi ya Uhuru kunyimwa ufadhili

Serikali imesema imeweka rekodi kwamba magari yanatiwa mafuta kupitia Master Card ya Ikulu

Muhtasari

•Alisema serikali ina rekodi za historia ya huduma ya utunzaji wa afisi ya Kenyatta iliyoanzia Mei 15, 2024.

•Msemaji wa serikali Isaac Mwaura katika taarifa iliyotolewa jioni alisema kuwa afisi ya Kenyatta imepewa magari 14 ambayo Ikulu huyapa mafuta na kuyatunza.

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura
Image: Hisani

Serikali ya Rais William Ruto imejitokeza kushughulikia kauli kali ya aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta kuhusu hadhi ya mafao yake ya kustaafu.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kupitia msemaji wake Kanze Dena Jumatatu alasiri aliwaambia wanahabari kwamba afisi yake imekabiliwa na njaa ya vifurushi vyake halali miongoni mwao mgao wa bajeti ulioainishwa, na kumlazimu rais huyo wa zamani kutekeleza miswada ambayo serikali inapaswa kushughulikia.

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura katika taarifa iliyotolewa jioni alisema kuwa afisi ya Kenyatta imepewa magari 14 ambayo Ikulu huyapa mafuta na kuyatunza.

"Pia walidai kwa uwongo kwamba kadi zao za mafuta zimezuiwa. Sisi, hata hivyo, tuliweka kwenye rekodi kwamba magari yanatiwa mafuta kupitia Master Card ya Ikulu. Rekodi zetu zinaonyesha kuwa magari kadhaa yalitiwa mafuta hivi majuzi kama Mei 15, 2024,” Mwaura alisema.

Alisema serikali ina rekodi za historia ya huduma ya utunzaji wa afisi ya Kenyatta iliyoanzia Mei 15, 2024.

“Ofisi pia ilisema kuwa magari hayo ni ya zamani na hayastahili Rais mstaafu. Lakini rekodi ziko wazi: Magari hayo yalinunuliwa katika miaka ya kuanzia 2020, 2021 na 2022. Kwa hivyo, yanafaa sana kwa Rais mstaafu ,” Mwaura alisema.

Kulingana na serikali, afisi ya Kenyatta imetuma ombi la magari manne yenye thamani ya Ksh.140 milioni.

Ofisi ya Kenyatta ilisema ilitengewa Toyota Land Cruiser mbili, Mercedes Benz na Range Rover iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Mkewe Rais Margaret Kenyatta, ambazo Dena alisema hata hivyo zilikuwa za zamani, kinyume na Sheria.

Kuhusu suala la hali ya afisi ya Kenyatta, Mwaura alisema afisi ya marehemu Rais Mwai Kibaki katika eneo la Nyari Nairobi ambayo aliitumia kati ya 2013 na 2022 na ambayo serikali ilinunua ni "ofisi inayofaa kwa Rais yeyote mstaafu."

"Kwa kukataa ofisi hii na kupendelea serikali kukodisha nyumba yake binafsi, rais mstaafu wa tatu anakaribisha serikali kukiuka sheria, kanuni na taratibu za manunuzi," alisema msemaji huyo wa serikali.

Alimshutumu Kenyatta kwa kutaka kuwa mwenye nyumba na mpangaji kwa wakati mmoja akiiita matukio ambayo serikali haiwezi kujihusisha nayo kwani huu ni mgongano mkubwa wa kimaslahi."

Vile vile, kwa wafanyikazi wa ofisi ya Kenyatta, Mwaura alisema majina ya George Kariuki na Kanze Dena hayajatumwa kwa mdhibiti wa Ikulu ili kushughulikiwa.

Alishikilia kuwa serikali ya Ruto inalipa kwa bidii mishahara ya rais mstaafu, wafanyikazi wake na marupurupu yao,hutia mafuta magari yake 14 na kurahisisha safari zake zote.

"Sheria inasema kwamba ni safari nne tu za nje ndizo zinazopaswa kulipwa kikamilifu na kwa muda usiozidi siku 14. Kuhusu riziki ya kila siku ukiwa kazini, Tume ya Utumishi wa Umma na kanuni za hazina ya Kitaifa hutumika,” alisema Mwaura.