Mamlaka ya kitaifa ya barabara kuu nchini Kenya imetangaza kutatiza kwa siku nne kwa trafiki ,katika barabara ya Mombasa.
Katika notisi ya Jumanne, Juni 11, KeNHA ilibainisha kuwa usumbufu huo wa muda utatokea katika barabara ya Mombasa,eneo la makutano ya Katani kati ya Juni 13 na Juni 16.
"KeNHA inawashauri madereva kufuata mpango uliopendekezwa wa usimamizi wa trafiki na kushirikiana na polisi na wakuu wa trafiki ambao watakuwa kwenye tovuti," Taarifa kutoka KeNHA ilisema.
Kulingana na mamlaka hiyo, usumbufu wa muda wa trafiki utaruhusu ujenzi wa msingi wa daraja la kati eneo hilo. KeNHA ilitoa mpango wa usimamizi wa trafiki ambao ungewaongoza madereva kwenye sehemu hiyo, na kuwataka kushirikiana na wasimamizi wa trafiki.
"KeNHA inawashauri madereva kufuata mpango wa usimamizi wa trafiki unaopendekezwa hapa chini na kushirikiana na polisi na wakuu wa trafiki..."
KeNHA na mamlaka ya barabara za mijini (KURA) wamekuwa wakifunga kwa muda sehemu za barabara jijini Nairobi kwa matengenezo kwa muda wa wiki chache zilizopita.
Mnamo Ijumaa, Mei 31, KeNHA ilitangaza kufungwa kwa muda kwa barabara ya Mombasa karibu na Imaara Mall kwa siku nne. Kufungwa kwa barabara hiyo ilikuwa ni kuwezesha kuwekwa kwa vizingiti vya kuzuia maji katika barabara.