Waandamanaji waharibu na kupora Klabu ya Mbunge Oscar Sudi Eldoret

Polisi walifika huku baadhi ya waandamanaji wakiingia kwenye kilabu na kuondoka na baadhi ya vitu

Muhtasari
  • Klabu hiyo ilifunguliwa rasmi wiki chache zilizopita wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Sudi na wabunge wengine kadhaa

Waandamanaji mjini Eldoret walivamia, kuharibu na kupora klabu moja mjini Eldoret inayohusishwa na mbunge wa kapseret Oscar Sudi.

Klabu hiyo inayojulikana kama Timber XO iko kando ya barabara ya Eldoret, Nairobi.

Klabu hiyo ilifunguliwa rasmi wiki chache zilizopita wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Sudi na wabunge wengine kadhaa

Waandamanaji hao waliandamana kutoka Eldoret CBD hadi kwenye kilabu ambapo walivamia na kuharibu kuta za vioo, madirisha na milango.

Polisi walifika huku baadhi ya waandamanaji wakiingia kwenye kilabu na kuondoka na baadhi ya vitu