Viongozi wa Kaskazini Mashariki wamfokea DP Gachagua kwa kumtaka Noordin Hajji kujiuzulu

Baada ya DP Gachagua kudai kwamba mkuu wa NIS Noordin Hajji anastahili kujiuzulu, viongozi hao wamejibu kwa kutishia kuanzisha mchakato wa kumbandua ofisini naibu wa rais.

Muhtasari

• Akihutubia wanahabari mjini Mombasa, DP aliyeonekana kughadhabika alilaumu NIS kwa maandamano ya sasa ya kuipinga serikali ambayo alisema yamesababisha vifo na uharibifu.

 
• Alisema kuwa NIS ilishindwa katika majukumu yake ya kumjulia hali mkuu wa nchi kabla ya wananchi kuingia mitaani.

DP Gachagua na mkuu wa NIS Noordin Hajji
DP Gachagua na mkuu wa NIS Noordin Hajji

Viongozi wa eneo la Kaskazini Mashariki wametishia kuanzisha mchakato wa kumbandua naibu wa rais kutoka mamlakani kisheria.

Wakizungumza Alhamisi siku moja baada ya Gachagua kumshambuli vikali mkurugenzi mkuu wa NIS, Noordin Hajji ambaye ni wa kutoka sehemu hiyo, viongozi hao walisema kwamba Gachagua anastahii kuachia ngazi kama naibu wa rais kwani anahujumu kazi na bosi wake.

Kulingana na viongozi hao, mashambulizi ya Gachagua yaliyoelekezwa kwa mkurugenzi wa NIS ni ya kukashifu urais, kwani ofisi ya NIS ni sehemu ya Baraza la Usalama la Kitaifa ambalo Gachagua pia ni sehemu yake.

“Naibu rais ni mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Baraza la Usalama badala ya kuchukua matatizo yake ili yaweze kushughulikiwa alichagua kuwahutubia maafisa wakuu wa serikali ambao kwa kawaida hawapaswi kujadiliwa hadharani Inasikitisha na hiyo inamaanisha kudhalilisha ofisi ya rais,” Mbunge wa Mandera Mashariki Abdullahi Bashir alisema.

Viongozi hao pia walimkosoa mkuu wa pili juu ya matamshi yake akisisitiza kwamba NIS haikulaumiwa kwa maandamano hayo.

Walimshutumu Gachagua kwa kujaribu kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila na kidini huku wakitishia kuwarai viongozi wengine bungeni kumbandua Gachagua.

Viongozi hao walitoa agizo kwa Naibu Rais wa kumtaka aondoke madarakani ikiwa hajafurahishwa na serikali na kufikiria kuanzisha kampeni za mapema za urais ili kumrithi Ruto 2027.

“Kama hafurahishwi na serikali mwache ajiuzulu katika utawala huu na ajiandae katika kinyang’anyiro cha 2027 ili agombee urais na iwapo atapendwa na watu wa Kenya tutaona anachokiendea. kufanya,” alisema Maalim.

Gachagua Jumatano alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) Noordin Haji ajiuzulu wadhifa wake ili kuandaa njia kwa Mkurugenzi Mkuu aliye na uwezo zaidi.

Akihutubia wanahabari mjini Mombasa, DP aliyeonekana kughadhabika alilaumu NIS kwa maandamano ya sasa ya kuipinga serikali ambayo alisema yamesababisha vifo na uharibifu.

Alisema kuwa NIS ilishindwa katika majukumu yake ya kumjulia hali mkuu wa nchi kabla ya wananchi kuingia mitaani.