Majeneza kadhaa yatapakazwa katikati mwa jiji la Nairobi na waandamanaji (video)

Baadhi ya waandamanaji walionekana wakitokea katika njia mbalimbali karibu na bustani ya Jevanjee wakiwa na majeneza hayo kabla ya kuyatelekeza katikati mwa barabara ya Moi Avenue.

Muhtasari

•   Tukio hili liliwaacha polisi kwa mshangao wasijue cha kufanya kwa mara moja kabla ya kuanza kuyainua na kuyaweka ndani ya lori moja la rangi nyeupe.

Majeneza ya maandamano
Majeneza ya maandamano
Image: X

Kisa kisicho cha kawaida kimeshuhudiwa mchana wa Jumanne katikati mwa jiji la Nairobi wakati waandamanaji waliamua kutapakaza majeneza Zaidi ya 10 kwenye barabara wakati wa maandamano yao.

Maandamano hayo ambayo yanaelekezwa dhidi ya serikali na haswa uongozi wa rais William Ruto, wengine wakishinikiza kung’atuka kwake madarakani kama rais.

Cha kushangaza ni kwamba wakati polisi wanhaha juu na chini kuwatuliza waandamanaji kwa kuwasambaratisha kwa kutumia vitoza machozi, wengine walitokea kusikojulikana wakiwa wamebeba majeneza na kuyaweka katikati ya barabara.

Tukio hili liliwaacha polisi kwa mshangao wasijue cha kufanya kwa mara moja kabla ya kuanza kuyainua na kuyaweka ndani ya lori moja la rangi nyeupe.

Baadhi ya waandamanaji walionekana wakitokea katika barabara mbalimbali karibu na bustani ya Jevanjee wakiwa na majeneza hayo kabla ya kuyatelekeza katikati mwa barabara ya Moi Avenue.