Mhubiri azuiliwa baada ya viungo vya mwili wa binadamu kupatikana garini mwake

Anasemekana kuwa mchungaji katika kanisa la mtaa wa Ndivisi, kaunti ya Bungoma .

Muhtasari

•Mhubiri mmoja anazuliwa na maafisa wa polisi baada ya sehemu za mwili wa binadamu kupatikana kwa gari lake.

•Wahudumu wa kuosha magari katika soko la Masikhu mjini Bungoma waligundua sehemu hizo za mwili kabla ya polisi kuitwa.

Pingu

Polisi katika kaunti ya  Bungoma wanamshikilia mtu mmoja anayefahamika kuwa  mhubiri ambaye alipatikana na sehemu za mwili wa binadamu kwenye gari lake.

Maafisa kutoka Webuye mashariki walisema kuwa sehemu za mwili zilipatikana zikiwa zimefichwa kwenye katoni na wahudumu wa kuosha magari katika soko la Masikhu mjini Bungoma.

Mshukiwa aliyetambulika kwa jina la Levis Simiyu, anasemekana kuwa mchungaji katika kanisa la mtaa wa Ndivisi. Mhudumu alikuwa akiosha gari kabla ya  kuona  mguu wa binadamu uliotokezea nje,ukiwa umeungua kwa kiasi.

"Kijana huyo aliacha kazi yake tayari kustaafu mapema, hadi meneja wa kituo cha mafuta alipotazama sanduku la kutisha," polisi walisema.

Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) iliongeza kuwa polisi waliitwa baadaye kwenye eneo la tukio.

“Meneja alitoa taarifa mara moja kwa polisi katika kituo cha Webuye, ambao walifika kwa wakati kabla ya mwenye gari kuondoka."

Viungo vya miili hiyo vimepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Webuye kwa uchunguzi zaidi.