logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC: Kaunti 7 za Kenya kuathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumatano

KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

image
na SAMUEL MAINA

Habari10 July 2024 - 05:13

Muhtasari


  • •KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Embu, Meru, Nyeri, Nakuru, Siaya, na  Isiolo.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 10. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Embu, Meru, Nyeri, Nakuru, Siaya, na  Isiolo.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kasarani Seasons na Runda Mimosa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Masinga na Ekalakala katika kaunti ya Embu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Kongo Acheke katika kaunti ya Meru pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Nyeri, sehemu za maeneo ya Kamatogu, Watuka, na shule ya upili ya Kirimara zitashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Barnabas na Mbaruk katika kaunti ya Nakuru pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Mbaga na Hawinga katika kaunti ya Siaya zitashuhudia kukatizwa kwa umeme katu ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Asili Millers katika kaunti ya Isiolo pia litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved