Sifuna apongeza hatua ya Rais kuwafuta kazi mawaziri wote

Mawaziri waliofutwa kazi ni pamoja na Kithure Kindiki wa Mambo ya Ndani, Moses Kuria(Utumishi wa Umma), Susan Nakhumicha (Afya)

Muhtasari
  • Kuvunjwa kwa baraza la mawaziri ni miongoni mwa mambo mengi ambayo Wakenya waliojitokeza barabarani kuandamana walikuwa wakiyapigia debe.
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna

Rais William Ruto amewafuta kazi makatibu wake wote katika baraza la mawaziri jambo ambalo limezua hisia tofauti miongoni mwa wakenya.

Akihutubia taifa, Rais Ruto alisema kuwa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri pekee na naibu wake Rigathi Gachagua ndio watakaosalia katika baraza la mawaziri.

"Nimeamua kuwafuta kazi mara moja makatibu wote wa baraza la mawaziri na mwanasheria mkuu wa Baraza la Mawaziri la Kenya isipokuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Masuala ya Kigeni," Ruto alisema."

Kuvunjwa kwa baraza la mawaziri ni miongoni mwa mambo mengi ambayo Wakenya waliojitokeza barabarani kuandamana walikuwa wakiyapigia debe.

Mawaziri waliofutwa kazi ni pamoja na Kithure Kindiki wa Mambo ya Ndani, Moses Kuria(Utumishi wa Umma), Susan Nakhumicha (Afya), Aden Dual(Ulinzi), Alfred Mutua(Utalii), Mithika Linturi(Kilimo) miongoni mwa wengine.

Katibu wa chama cha ODM na seneta wa Nairobi Edwin Sifuna alionekana kupongeza hatua ya Rais.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa X seneta huyo alisema kwamba kuwafuta mawaziri wote kazi ni mwanzo mzuri.

"Kuwafuta kazi Makatibu wote wa Baraza la Mawaziri ni mwanzo mzuri."