logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kalonzo afichua mpango wa kuunda chama kipya cha kisiasa

Alisema kwamba Azimio itapinga mipango yoyote ya kumng’oa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoka wadhifa wake.

image
na Samuel Maina

Habari06 August 2024 - 07:06

Muhtasari


  • •“Jiunge na harakati mpya tunayozindua. Usifanye makosa, Rais wa zamani Uhuru Kenyatta yuko pamoja nasi,” alisema Kalonzo.
  • •Alisema kwamba Azimio itapinga mipango yoyote ya kumng’oa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoka wadhifa wake.

Sehemu ya viongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya imethibitisha mipango ya kuunda chama kipya cha kisiasa kilicho na lengo la kuwa na mwelekeo tofauti na serikali pana iliyotangazwa hivi majuzi na Rais William Ruto.

Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka, alifichua hayo alipokuwa katika Kaunti ya Kiambu, na kuongeza kuwa kuundwa kwa chama hiki kipya cha kisiasa kumepata baraka za Rais wa mstaafu Uhuru Kenyatta.

“Jiunge na harakati mpya tunayozindua. Usifanye makosa, Rais wa zamani Uhuru Kenyatta yuko pamoja nasi,” alisema Kalonzo katika jitihada zake za kuhamasisha wakazi wa Mlima Kenya kuunga mkono chama kitakachotangazwa baadaye.

Katika kampeni yake, makamu wa rais huyo wa zamani pia anawaahidi wananchi wa eneo la Kati ya Kenya kwamba Azimio itapinga mipango yoyote ya kumng’oa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoka wadhifa wake.

Kundi lililoongozwa na Kalonzo ambalo pia lilijumuisha Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee, Jeremiah Kioni na kiongozi wa DAP Kenya, Eugene Wamalwa, wanaamini kuwa ni wakati wa kuondoka kutoka Azimio baada ya Chama cha ODM cha Raila Odinga kukubaliana kufanya kazi na utawala wa Rais William Ruto.

Baadhi ya washirika wa Odinga wamependekezwa na Ruto kuhudumu katika Baraza lake la Mawaziri na sasa wanangojea kuidhinishwa na wabunge kabla ya kuanza kazi.

“Mwenye tumeachiwa sasa na mwenye tunatembea naye kwa sababu lazima kuwe na mbadala wa mambo yanayofanyika katika nchi hii ni Kalonzo.

Sisi wakazi wa eneo hili (la Mlima Kenya) tufungue macho. Sisi tukitembea na Kalonzo tunaomba Mungu mapenzi yake yafanyike,” alisema Jeremiah Kioni wa Chama cha Jubilee.

“Mheshimiwa Kalonzo Musyoka, wewe ongoza sisi wote turudiane, tutengeneza ile GEMA ya mbeleni,” aliongeza aliyekuwa Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved