Maandamano, baadhi ya wakenya wamtaka mkuu wa majeshi kuwalinda

Kwenye barua hiyo wakenya hao walieleza ghadhabu yao ya jinsi polisi wamekuwa wakiwakabili kila wanapoandamana.

Muhtasari

•Wakimuandikia waraka mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Kenya (CDF) bwana Charles Kahariri ili aweze kuingilia kati na kuhakikisha wakenya hawadhulumiwi wala kutekwa nyara

•Wamemujulisha Bwana Charles kuwa watakuwa wakijughulisha katika maandamano hayo kwa amani

Rais William Ruto akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi marehemu Francis Ogolla (kulia) na Makamu mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Lt Jenerali Charles Kahariri mnamo Machi 9, 2024.
Rais William Ruto akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi marehemu Francis Ogolla (kulia) na Makamu mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Lt Jenerali Charles Kahariri mnamo Machi 9, 2024. Rais William Ruto akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi marehemu Francis Ogolla (kulia) na Makamu mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Lt Jenerali Charles Kahariri mnamo Machi 9, 2024.
Image: MAKTABA

Kauli mbiu #nanenanemarch imezidi kupamba moto mtandaoni huku baadhi ya wakenya wakimuandikia waraka mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Kenya (CDF) bwana Charles Kahariri ili aweze kuingilia kati na kuhakikisha wakenya hawadhulumiwi wala kutekwa nyara wanapojishirikisha katika kufanikisha haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kuandamana.

Kwenye barua hiyo wakenya hao walieleza ghadhabu yao ya jinsi polisi wamekuwa wakiwakabili kila wanapoandamana.

Baadhi ya masuala  yaliyotiliwa mkazo ni pamoja na utekaji wa kimabavu wa wananchi wa hivi punde.

Barua aliyoandikiwa Bwana Charles Kahariri
Image: HISANI

Katika video zinazosambaa mitandaoni ya hivi punde, mkenya mmoja ambaye mpaka sasa hajabainika ni nani amenekana kutekwa nyara na kundi la watu wasiojulikana.

Watu hao wanaonekana wakiwa wamebeba bunduki na wanatembea na magari mawili.

Mbali na hayo, wamemujulisha Bwana Charles kuwa watakuwa wakijughulisha katika maandamano hayo kwa amani na kwamba wanafanya hivyo ili kujibisha serikali kuhusiana na ufisadi, uhaba wa kazi miongoni mwa vijana na kadhalika.

Pia, walieleza kuwa baadhi ya polisi wamekuwa wakiwadhulumu kwa kutumia vitoa machozi na kutumia risasi za kuua ambazo zimeleta vifo kwa wananchi takriban sitini.

Walieleza ghadhabu zao za jinsi polisi wamekuwa wakitumia nguvu zaidi kinyume na Sheria ya korti iliyo wazuia kutumia mitindo kama hiyo kila wananchi wanapoandamana.

Walimaliza wakiwashukuru maafisa ulinzi wa Kenya (KDF) kwa kuwa wenye maadili na utu hasa kwenye maandamano ya mwisho ambap maafisa hao walionekana kwa video mbalimbali wakiwasindikiza waandamanaji hadi manyumbani.

Walimaliza wakiwarai KDF kuendeleza hali hiyo ya juu kila wanapojishirikisha kazini.