Mwanamke ameza sindano ya kushona - Kirinyaga

"nina uchungu mwingi kooni na siwezi nikala chochote" Everline asema.

Muhtasari

•"Tuna hofu yakua huenda tukampoteza.

• Naomba msaada ili mke wangu apate matibabu

EVERLINE KAREKIA
EVERLINE KAREKIA
Image: EVERLINE KAREKIA //KENYA NEWS

Mwanamke mwenye umri wa miaka 31 kwa jina la Erveline Kareika kutoka  kijiji cha Mugambaciura kaunti ya Kirinyaga, ameshangaza wengi kwa kudai kumeza sindano ya kushona nguo.

Everline alisema anapitia kipindi kigumu na kwamba bado hajapata matibabu yoyote na kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema kufadhili matibabu yake.

 Mumewe Kelvin Maina ,kwa mahojiano na wanahabari ,alisema kuwa kisa hiki kilitendeka wakati alipokua akimlisha mwanawe wa miezi minane, alipomaliza kushona na kueka sindano kwenye kinywa chake na kisha kuumeza kwa ghafla.

Aidha ,Maina asema hatua yake ya kumpeleleka mkewe hosipitalini huko Embu haikuzaa matunda   licha ya kulipa sh.800 ili kufanyiwa x-ray.

Vilevile bwana Maina anasema haikua safari ya mwisho na kwamba walichukua hatua ya kwenda Kerugoya ambapo walitozwa sh.10,000 ambazo hakua nazo nakulazimika kuridi nyumbani huku sindano ikiwa imekwama kwa koo ya bibiye.

"Tuna hofu kuwa huenda tukampoteza na kwa hivyo  ndiposa naja kwenu kuomba msaada ili apate matibabu zaidi" Maina alisema kwa huzuni.