•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Elgeyo Marakwet, Homa Bay, Embu, Kwale na Nyeri.
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Agosti 21.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Elgeyo Marakwet, Homa Bay, Embu, Kwale na Nyeri.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Golfcourse na Kibera zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Soko la Katalel katika kaunti ya Elgeyo Marakwet litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Kandiege, Kanyamfwa na Andhiro katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Machanga, Ngiori, na Makima katika kaunti ya Embu pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Gatondo, Karichen, Gatuamba na Itundu yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Mwangwei na Lungalunga katika kaunti ya Kwale pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.