KNEC kuwaandalia wanasoka 8 wa Junior Starlets mtihani spesheli

Hatua hii imefikiwa baada ya timu hiyo kutarajiwa kuwakisha Kenya kwenye kombe la dunia katika Taifa la Dominica Republic mwezi wa 10.

Muhtasari

• Hatua hii imefikiwa baada ya timu hiyo kutarajiwa kuwakisha Kenya kwenye kombe la dunia katika Taifa la Dominica Republic mwezi wa 10.

•Hatua hii imefanishwa na ushirikiano baida ya baraza la kitaifa la Mtihani ,wizara ya michezo na Shirikisho la soka FKF.

JUNIOR STARLETS
JUNIOR STARLETS
Image: JUNIOR STARLETS//FKF FACEBOOK

Baraza la kitaifa la mitihani KNEC limesema litawaandaliwa wachezaji 8 wa timu ya taifa ya kina dada wasiozidi umri wa miaka 17 mitihani spesheli.

Wachezaji hao 8 ni miongoni mwa wanafunzi watakaotarajiwa kuketi katika mitihani ya kitaifa miezi miwili ijayo lakini wakati uo huo wanatakiwa kusafiri na timu ya taifa, Junior Starlets kuelekea Dominican Republic kwa ajili ya mashindano ya kombe la dunia ya kina dada wasiozidi umri wa miaka 17.

Ni jambo ambalo lilichangiwa pakubwa na MP Irene Mayaka ambapo alileta ombi hilo kwa Serikali  ili waweze kuwekewa mtihani spesheli baada ya michuano hiyo kutokea wakati mmoja na mtihani wa kitaifa .

Baraza hilo hapo awali ilikuwa imesema kuwa wachezaji hao ikiwa wanataka kushiriki katika michuano hiyo ya kombe la Dunia kwa U17,michuano itakayo andaliwa katika taifa la Dominica Republic mwezi wa 10,ni labda waghairi mtihani huo na waurejelee mwaka ujao.

Hatua hiyo imefanikishwa na ushirikiano wa wizara ya hiyo ya Elimu chini ya waziri Julius Ogamba,ile ya michezo chini yake Kipchumba Murkomen pamoja na shirikisho linalo simamia soka apa Kenya FKF linaloongozwa naye Nick Mwendwa.

Junior Starlets wamo katika kundi C ambapo ni kundi ambalo linatarjiwa kuwa na ushmdani mkali ,baada yakuwa na Taifa kama Korea,Mexico na England.

Mildred Cheche ,ni kocha mkuu amesema kuwa timu hiyo inazidi kuzanya mazoezi na wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo.