•KPLC imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
•Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi na Homabay.
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Agosti 26..
Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi na Homabay.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Lower Kabete zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Woibero na Ojunge katika kaunti ya Homa Bay pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.