Fahamu kaunti 7 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Alhamisi

Maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisii, Kilifi, Migori, Kiambu, Mombasa, na Kajiado.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Agosti 29. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisii, Kilifi, Migori, Kiambu, Mombasa, na Kajiado.

Katika kaunti ya Nairobi, maeneo ya Kibarage Way, Sewage, Kibiku, Joska, Utawala, Njiru, Vicken na North Impact yataathirika na kukatizwa kwa stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kegati, Riambanyi na Kiogoro katika kaunti ya Kisii yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Mtondia, Tezo, na Chumani katika kaunti ya Kilifi yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Migori, maeneo ya Namba na Isebania yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kibichoi, Komothai Boys, Marion School, na mji wa Gatundu katika kaunti ya Kiambu yataathirika kati ya saa mbili unusu na saa saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Miritini na Jomvu katika kaunti ya Mombasa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za mji wa Kitengela katika kaunti ya Kajiado pia zitakosa umeme kati ya saa mbili na saa kumi na moja jioni.