• Kwa upande wake, rais Ruto aliahidi kumpigia kampeni Raila Odinga kote Afrika ili kuhakikisha anatua kiti cha mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika, AUC.
Rais Ruto hatimaye ametoa shukrani zake sufufu kwa kiongozi wa ODM, Raila Odinga kwa juhudi zake za kumsaidia kuliunganisha taifa wakati maandamano ya vijana wa Gen Z yalitishia kuleta mgawanyiko nchini.
Akizungumza katika kaunti vya Kisumu katika siku yake ya mwisho ya kuhitimisha ziara ya kimaendeo ya Luo Nyanza, rais alimtaja Odinga kama kaka mkubwa ambaye ana maslahi ya taifa la Kenya katika moyo wake.
“Mimi nataka nimshukuru ndugu yangu mkubwa Raila Odinga kwa kukubali sisi sote tuweke tofauti zetu kando na kuangalia umoja wa Wakenya, stability, security na progress ya nchi yetu. Raila Odinga najua umewahi kuwa mpinzani wangu, najua umewahi kuwa kiongozi wangu wa chama, lakini leo tunasimama pamoja bega kwa bega kwa ajili ya Kenya, na nakupigia saluti kama mkenya mzalendo mwenye maslahi ya nchi moyoni,” Ruto alisema.
Ruto na Raila waliweka tofauti zao pembeni na kuamua kufanya kazi pamoja, ODM ikichangia mawaziri 4 katika serikali mpya jumuishi, kufuatia kuvunjwa kwa baraza la mawaziri la Kenya Kwanza mapema mwezi Julai.
Kwa upande wake, rais Ruto aliahidi kumpigia kampeni Raila Odinga kote Afrika ili kuhakikisha anatua kiti cha mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika, AUC.