Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya amewashauri wanaume kutoona haya katika kulia wakati mambo yanawaendea segemnege katika maisha.
Katika video moja ambayo imekiuwa ikipiga misele katika mitandao ya kijamii, gavana Natembeya alisema kwamba ni vizuri kulia wakati mtu ako na stress na kuwashauri wanaume kulia ili kupunguza mawazo mengi wakati wa changamoto.
“Boychild, unajua katika tamaduni zetu, mwanaume hatakikani kuonyesha ile weakness eti unalia, ama unateta na kulalamika. Unataki uweke sura ya kazi wakati mwingi. Ndiposa unapata wanaume wanapitia changamoto nyingi sana lakini pia hawaongei. Ningependa kuwashauri wanaume tu wawe wawazi katika kuonyesha hisia zao. Sio vibaya kuonyesha hisia,” Natembeya alishauri.
“Wakati mwingine hata lia tu kama mambo ni mabaya. Hakuna jambo baya hapo, kwa sababu ukitoa emotions unaheal. Ndiposa mnaona wanawake wanaishi miaka mingi kwa sababu wao wakipata jambo lolote wanaitana na kukaa chini na kuongea, lakini mwanaume unajifungia kwa kona peke yako. Unanuna na kuenda kubugia pombe, utakufa,” aliongeza.
Natembeya alisema kwamba wakati akiwa katika maisha ya awali kama mkuu wa mkoa wa bonde la ufa, alikuwa anapata visa vingi vya wanaume kujitoa uhai na wengine kudhulumiwa hata kingono.