Gavana Sakaja atangaza nafasi 20,000 kwa vijana za kazi mtaani

Sakaja alisema kazi mtaani inarejea ila kwa jina tofauti na mbinu tofauti ya kufanya kazi

Muhtasari

•Kazi mtaani inarejea lakini kwa jina la 'Climate Works Mashinani'

•Mradi huo ni tofauti kidogo na wa kazi mtaani kwa kuwa vijana watafanya kazi kwa siku kumi kisha kuhudhuria mafunzo siku zingine kumi

Vijana wakisafisha mtaa
Vijana wakisafisha mtaa
Image: Facebook

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘Dishi na County’ katika shule ya msingi Umoja 1 Jumatatu Septemba 2, Sakaja alisema kuwa kazi mtaani inarejea.

Sakaja alisema kuwa kazi mtaani inarejea lakini kwa jina tofauti Climate Works Mashinani kwani rais alisikiza vijana.

Kulingana na Sakaja, mradi huo ni tofauti kidogo na wa kazi mtaani kwa kuwa vijana watafanya kazi kwa siku kumi kisha kuhudhuria mafunzo siku zingine kumi na watalipwa na serikali.

" Watu wa Nairobi kazi mtaani inarudi...vijana tunaanza na 20,000 ambao watapata kazi...mdosi aliskiza,"Sakaja.

“Kwa kila ward MCAs tupange vijana, tupange vijana ambao watakuwa wanafanya kazi siku kumi na hizo siku kumi zingine wanaenda training” Sakaja aliongeza.

Kazi Mtaani ni mpango wa kitaifa ambao ulizinduliwa Aprili mwaka wa 2020 ili kusaidia vijana kupata uwezo wa kujikimu kimaisha baada ya janga la Corona. Katika mradi huo, vijana walikuwa wanashiriki katika zoezi ya kusafisha mazingira na wangelipwa mwisho wa wiki.