•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nakuru, Kisumu, Kisii, Murang'a, na Kiambu.
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Septemba 3.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nakuru, Kisumu, Kisii, Murang'a, na Kiambu.
Katika kaunti ya Nairobi, maeneo ya General Mathenge na Eldama Ravine yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja usiku.
Maeneo ya Soilo na Kabarak katika kaunti ya Nakuru yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Kombewa na Ober Kamoth yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu ya mji wa Kisii katika kaunti ya Kisii zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Murang'a, maeneo ya Thika Greens na Delview yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Kinoo na Muthiga katika kaunti ya Kiambu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja asubuhi.