Bosi wa zamani wa KEMRI Dr.Davy koech ameaga dunia

Mwanasayansi na bosi wa zamani wa taasisi ya KEMRI aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Muhtasari

•Mwanzilishi na muhudumu wa taasisi ya utafiti wa tiba ya Kenya (KEMRI) ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73 kufuatia kuugua kwa kipindi kirefu.

Dr.Davy Koech
Image: hisani

Aliyekuwa mkuu wa taasisi  ya utafiti wa dawa nchini Kenya (KEMRI), daktari Davy Koech ameaga dunia.

Koech, kulingana na taarifa za familia, inasemekana alifariki siku ya Alhamisi 5, Septemba 2024, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Aidha, familia haijatoa taarifa zaidi kuhusu kifo chake. Koech,ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73.

Koech alikuwa mzoefu katika elimu ya kinga na atakumbukwa kwa mchango wake wa juu kwenye taasisi hiyo weakati wa kuibuni.

Akiwa na umri wa miaka 23, Koech, aliogoza mchakato wa ufadhili ili kuianzisha taasisi hiyo, na ambayo kwa sasa inafanya vyema katika afya ya kibanadamu dhidi ya maradhi na kubuni dawa mpya ili kupigana na maradhi ibuka.

Koech, baada ya kupata cheti cha shahada ya shahada ya sayansi kwenye kemia na zoolojia, akiwa chu kikuu cha Nairibi, mnamo Aprili 1974, alizamia katika swala la shahada ya pili kwenye taaluma ya dawa hususan kwenye kiafya,katika chuo kikuu cha Duquesne, Pennsylvania.

Akiwa anashughulikia cheti chake cha uzamifu, Koech na wenza wake, ikiwemo Prof. Kihumbu Thairu na Prof.Mutuma Mugambim, walikuwa wanashughulikia changamoto ya ukosefu wa mtaala wa utafiti katika shule ya kimafunzo ya udaktari,Nairobi.

Walichangia pakubwa uundwaji wa mwongozo wa taasisi ya utafiti  chuoni humo,kabla ya kuchukua idhinisho la kisayansi na teknolojia wmwaka wa 1977 kupitia  mwanasheria mkuu,Generali.Charles Njonjo.

Tatizo kubwa likuwa kupata ufadhili ambao ulikuwa chuni ya uungwaji mkono na serikali ya Japan.

Katika mwaka wa 2021, Koech alipatikana na hatia na koti kwa swala la ufisadi wa kusambaza kima cha shilingi milioni 19.3 ambazo zilkuwa zimetengewa Kaonti ya Kisumu ili kuzuia maambukizi ya maradhi,kwa akaonti yake yeye binafsi.Na ambapo aliamrisha kuziregesha ama kifungo cha miaka sita gerezani.Na kwa maana akuwa na uwezo wa kuzipata,alifungwa jela.

Licha ya kifungo hicho,baada ya Rais dr.Ruto kuchaguliwa,mnamo 2023, Ruto aliagiza kuachiliwa huru kwa mwanasansi huyo