Kenya Power yatoa taarifa kuhusu kupotea kwa stima katika sehemu kubwa ya nchi

KPLC) imefahamisha taifa kuhusu kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Muhtasari

•"Tunaomba radhi kwa usumbufu na tunaomba uvumilivu wako kwani wahandisi wetu wanafanya kazi haraka kurejesha huduma," KPLC ilisema.

Image: MAKTABA

Kampuni ya kusambaza umeme nchini, Kenya Power & Lighting Company (KPLC) imefahamisha taifa kuhusu kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Katika taarifa yake Ijumaa asubuhi, kampuni hiyo ilibainisha kuwa kumekuwa na hitilafu ya umeme katika sehemu kadhaa isipokuwa sehemu za maeneo ya North Rift na Magharibi mwa Kenya.

Wasambazaji umeme waliomba radhi kwa wateja wao na kuwahakikishia kuwa juhudi za kurejesha uhusiano zinaendelea.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu na tunaomba uvumilivu wako kwani wahandisi wetu wanafanya kazi haraka kurejesha huduma," KPLC ilisema.

Pia walibaini kuwa masasisho yatatolewa kadri mchakato wa kurejesha nguvu ukiendelea.

Hii ni mara ya pili ambapo huduma za umeme zinatatizika katika sehemu kubwa ya nchi katika kipindi cha wiki moja iliyopita.