KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumamosi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Septemba 7.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Uasin Gishu na Trans Nzoia.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Septemba 7. 

Katika taarifa ya Ijumaa jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Uasin Gishu na Trans Nzoia.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, maeneo ya Semtech Factory, Safaricom Booster, Jua Kali, Wood Treatment, Ngamia Petro, Kakasia Chemist, Police Post na Viunga vyake yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Endebes, na Panacol katika kaunti ya Trans Nzoia pia zitakosa umeme kati  ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.