Kaunti 7 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Alhamisi- KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Septemba 5.

Muhtasari

•Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Nairobi, Bomet, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet,Kirinyaga, Meru, na Kiambu.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Septemba 5. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Bomet, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet,Kirinyaga, Meru, na Kiambu.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Ridgeways zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Siongiroi na Labotiet katika kaunti ya Bomet yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Endebes na Panocal katika kaunti ya Trans Nzoia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kapcherop, Chebai, na Kibigos katika kaunti ya Elgeyo Marakwet yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kirinyaga, sehemu za Baricho na Njeru Githae zitakuwa bila umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Akaiga na Kunati katika kaunti ya Meru pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Posta, Terrasol, Gathatha Road, Munyu Dispensary, Karuri, Banana, na Ndenderu pia zitaathirika.