Mvulana ajitia kitanzi,baada ya kuzuiwa kuuza ng'ombe

Mvulana mmoja kutoka kaunti ya Migori alijitoa uhai baada ya kuzuiliwa kuuza ng'ombe bila ruhusa ya babake katika kijiji cha Mawini

Muhtasari

•Mvulana mmoja alijitia kitanzi katika kaunti ya Migori kuhusiana na kuzuiliwa kuuza ng'ombe bila kitambulisho cha babake.

•Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika makafani ya hosipitali ya Migori Level Four,huku ukisubiri upasuji ili kubaini chanzo cha kitendo hicho.

Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI

Polisi katika kaunti ya Migori wanaendelea kuchunguza kwa kina kuhusiana kisa cha mvulana mmoja wa miaka 17, kujitia kitanzi ,baada ya kuzuiliwa kuuza ng'ombe bila idhini ya babake mzazi,masaa machache baadae.Janga hili lilitokea katika kijiji cha Mawini 

Kuhusiana na taarifa ya mdogo wa chifu katika kata ndogo ya Nyamaharaga,Rose Ooko,alivo hojiwa na kituo kimoja cha televisheni umu nchni,alisema kuwa ,mwili wa mwendazake ulipatikana ukiwa unaning'nia katika chaka moja karibu na boma,masaa machache baada ya mvulana huyo kuzuiwa kuuza ng'ombe huyo bila kitambulisha rasmi cha babake.

Aidha,mwendeazake baada ya kutokuwa na uwezo wa kuuza ng'ombe bila kitambulisho cha babake,aliagiza mnunuaji ampe dakika chache ili arejee nyumbani kuleta kitambulisho ,lakini hakurejea tena,baadae mwili wake ulipatikana ulening'inia kwa kamba mtini.

Ooko ,alisema bado hawajabaini chanzo kamili cha mvulana kupelekea kutoa uhai wake.Aidha,Ooko aliuliza kama uenda mvulana huyo alijitoa uhai kwa kuogopa aghabu ambayo angepokea kutokana na kitendo hicho kutoka kwa babake.

Sasa familia hiyo sasa imeghubikwa na huzuni huku wakisema ni jambo ambalo si la msingi mtoto wao kujitia kitanzi,na jambo ambalo wangesuluhisha kama familia.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika makafani ya Hosipitali ya Migori Level Four,huku ukusubiria upasuaji ili kubaini chanzo kamili na uchunguzi wa polisi.

Swala hili linajiri ambapo dunia inaadhimisha mwezi wa kuklabiliana na visa vya kujitia kitanzi,huku asilimia kubwa ikiwa ni ya vijana.Aidha,inazidi kuongeza visa vya kujitia kitanzi kaunti humo.

 

Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI
Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI