Kumbuka ahadi zetu kwa wafanyabiashara, Gachagua amwambia Sakaja

Wafanya biashara wapinga kuhamishwa hadi soko jipya la barabara ya Kangundo

Muhtasari

• Naibu wa rais amemkumbusha gavana Sakaja kuhusu maagano walioweka na wafanyabiashara wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2022.

•Gachagua amemshauri Sakaja kufanya kikao na usimamizi wa soko la Wakulima kutatua swala hilo.

Polisi waeusha vitoa machozi kwa waandamanaji wa soko la Wakulima Alhamisi 12, Septemba 2024
MAANDAMANO Polisi waeusha vitoa machozi kwa waandamanaji wa soko la Wakulima Alhamisi 12, Septemba 2024
Image: image: THE STAR

Naibu wa rais Rigathi Gachagua amemshauri gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja kuwasikiza wafanyabiashara wa soko la Wakulima jijini Nairobi.

Kupitia mtandao wake wa X, naibu wa rais amesema  wafanyabiashara hao wamempigia simu na kumkumbusha ahadi waliotoa kwao.

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022, Gachagua amemkumbusha Sakaja jinsi alivyompigia debe kwa wafanyabiashara hao eneo la Muthurwa.

"Tuna ahadi kuwa utawala wetu hautawai vuruga maisha ya wafanyabiashara hawa wala kurudisha chini uchumi wao." aliandika Gachagua.

Wafanyabiashara wa  soko la Wakulima waliandamana Alhamisi asubuhi kwa kufunga barabara za Jogoo na Haile Sellasie kulalamikia kuondolewa sokoni.

Usimamizi wa kaunti ya Nairobi inapanga kuhamisha wafanyabiashara hao hadi soko jipya lililojengwa karibu na barabara ya Kangundo.

Kulingana na utawala wa kaunti ya Nairobi, unahofu kuwa soko la barabara ya Kangundo litasaidia kupunguza uchafu mjini na kusaidia kuboresha mazingira ya jiji kuu la Nairobi.

Kwa upande wa wafanyabishara hao walioandaa maandamano, wamedai kuwa tayari sehemu za kuuzia katika soko jipya tayari limejaa. wamesema kuwa soko la wakulima ndilo linalisha wakaazi wote wa Nairobi na nje ya Nairobi.

Aidha, naibu wa rais amemrai gavana Sakaja kufanya kikao na usimamizi wa soko la Wakulima ili kupata mwafaka wa mabadiliko wanayolenga kutekeleza bila kuathiri maisha ya wafanyabiashara hao.

Naibu wa rais pia ameomba radhi bwana Sakaja ikiwa atahisi(Sakaja) atahisi kukwera na wosia wake. "Tafadhali naomba msamaha ikiwa nimekukwaza, lakini wanakuja kwangu kwa sababu nilikuwa mdhamini wako kwa maswala ya uaminifu. Tafadhali ndugu yangu." Aliandika Gachagua.