Wanafunzi 6 wafariki katika ajali kwenye barabara ya Kitui-Kibwezi

Baada ya tukio hilo, dereva wa gari hilo alitoweka na baadae akajisalimisha katika kituo cha polisi cha Mutomo.

Muhtasari

• Wanafunzi hao walikuwa njiani kuelekea shuleni wakati mkasa huo ulipotokea.

•Ajali hiyo inatokea wakati wakenya bado wanaomboleza vifo vya zaidi ya wanafunzi 21 katika kisa cha moto katika shule ya  Hillside Endarasha iliyoko Nyeri.

Ajali
Ajali
Image: HISANI

Wanafunzi sita walifariki Ijumaa asubuhi baada ya kugongwa na gari ambalo halikusimama kwenye barabara ya Kitui - Kibwezi.

Inasemekana  wanafunzi hao walikuwa njiani kuelekea shuleni wakati mkasa huo ulipotokea.

Akithibitisha tukio hilo Naibu  Kamishna wa kaunti Vincent Loctary Lomachary alisema waathiriwa walikuwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Kulingana na Lomachary sita hao waligongwa na gari aina ya Probox na kupoteza maisha papo hapo wakati walikuwa wakivuka barabara.

Baada ya tukio hilo, dereva wa gari hilo alitoweka na baaadae akajisalimisha katika kituo cha polisi cha Mutomo.

Wakati uo huo,gari husika limevutwa na askari huku uchunguzi ukiendelea kubaini tukio hilo zaidi.

Ajali hiyo inatokea wakati wakenya bado wanaomboleza vifo vya zaidi ya wanafunzi 21 katika kisa cha moto katika shule ya  Hillside Endarasha iliyoko Nyeri.