Wanne wafariki baada ya bomba la maji taka kuanguka-Shauri Moyo

Wanne wapoteza maisha yao bada ya bomba la maji taka kuanguka katika mtaa wa shauri moyo

Muhtasari

•Watu wanne wamefariki baada ya kuangukiwa na bomba la maji taka katika mtaa wa shauri Moyo,Nairobi.

•Msemaji wa shirika la huduma ya polisi Dr Resila Atieno Onyango amedokeza kuwa watatu wameweza kuokolewa na kupelekwa katika hosipitali ya Mama Lucy kwa matibabu zaidi.

•Msemaji huyo amesema kuwa bado ni zoezi ambalo linaendelea ili kuzuia maafa zaidi.

•Bomba hilo la maji taka lilikuwa bado linaendea kuchimbwa kabla ya kuanguka.

SHUGHLI ZA UOPOAJI, SHAURI MOYO.
Image: HISANI

Watu wanne wamepoteza maisha Ijumaa baada ya bomba la maji taka ambalo bado lilikwa linaendelea kuchimbwa kuanguka katika mtaa wa shauri moyo ,Nairobi na kusababisha maafa hayo.

Waliofariki walikuwa wafanyakazi ambao walikuwa wakijenga bomba la  maji taka,baada ya kuta zake kuporomoka.

Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu, watu watatu wameokolewa katika mkasa huo na kupelekwa katika hosipitali ya Mama Lucy,ambapo wanaendelea kupata matibabu zaidi  kufuatia ushirikiano wa zimamoto kaunti ya Nairobi,gari za dharura za NMS na pia vile vile Kenya Police.

Akizungumza na wanahabari, msemaji wa polisi,Dr Resila Atieno Onyango amesema kuwa shughli za uokoaji zinaendelea ili kuzuia maafa zaidi katika eneo husika.

Alisema kuwa kwa sasa wameweza kuopoa miili minne katika eneo hilo na wakaweza kuopoa watu watatu wakiwa salama,"tumetoa miili minne ya maiti katika tukio hili baada ya bomba hili kuanguka,vile vile tumeweza kuwaokoa watatu ambao wako salama na kwa sasa wanazidi kupokea matibabu ".

Aidha,msemaji huyo alisema kuwa shughli za uopoaji zinaendelea, zoezi ambalo linaongozwa na kamati ya ulinzi na usalama.