Mgawanyiko wazidi kushuhudiwa eneo la Mlima Kenya

Baadhi ya viongozi kutoka Mlima Kenya mashariki sasa wamethibitisha kumuunga mkono Kithure Kindiki.

Muhtasari

•Wameseme wataaunga mkono waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki mkono kama daraja la kufikisha matakwa ya eneo la mlima Kenya kwa Rais.

ELDERS PRESS CONFERENCE
Image: HISANI

Viongozi takribani 500 kutoka eneo la mlima Kenya hususan katika kaunti za Meru, Embu na Tharaka Nithi,walionekana kuvunja uhusiano wao na naibu rais Rigathi Gachagua,na kuthibitisha kuwa sasa wataaunga mkono waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki mkono kama daraja la kufikisha matakwa ya eneo la mlima Kenya kwa Rais.

Katika taarifa kwa wanahabari,katika eneo la Embu, viongozi hao walisema kuwa wanatambua jitihada za rais katika juhudi za kuimarisha na kuleta uendelevu nchini, lakini wakaeleza kuwa hofu yao kubwa ni mvutano wa kisiasa ambao unazidi kuzuka kwa kasi.

"Mvutano huu unazuia shughuli  nyingi sana za maana, kama ukamilishaji wa miradi,kuinua uchumi hasa kwa wakulima na vile vile kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana. Kile ambacho tungetaka ni viongozi wote wakumbatie umoja na kutilia uendelevu kipau mbele bali sii kutoa maneno ya kugawanya wananchi," Alisema Cyrus Ngeranwa.

Aidha, walisema kuwa ili kuhakikisha kwamba miradi ya eneo hilo imo salama, sasa wamemthibitisha waziri wa ulinzi wa ndani Prof. Kithure Kindiki kuwa daraja litakalo fanikisha uhusiano mwema na rais, na kupelekea miradi ya eneo hilo kumalizika kwa mapema na kufaidi wakaazi.

"ili kufanisha miradi ya eneo hili,na kuakikisha tunabakia na lengo la uendelevu,sasa tunamthibitisha Prof. Kithure Kindiki kuwa daraja kumfikia Ruto pamoja na serikali yake,na tunaaminia kuwakulingana na mwonekano wake wa kitaifa,atatusaidia kuleta uhusiano mwema na maeneo mengine,"

Viongozi hao wanamuunga mkono Prof Kindiki baada pia ya kundi la vijana kutoka eneo hilo mashariki kuthibitisha kuunga mkono Kindiki kwenye suala ilo.

Vijana hao, walimtaja Kindiki kama kiongozi ambaye ana lengo la kufanya taifa la Kenya kuwa lisilo la kikabila,chuki na mgawanyiko.

"Tunaunga mkono swala la kumteua Prof. Kindiki kuongoza eneo la mlima kenya mashariki katika mazungumzo ya kitaifa ambayo yataleta uendelevu kwa Taifa", Kiongozi wa vijana alisema katika taarifa kwa wanahabari.

Katika wiki iliyopita mkutano ulifanyika katika kaunti ya Laikipia, ambapo wabunge 40 kutoka  eneo hilo la Mlima Kenya magharibi wakiwa pamoja na diaspora walisaini makubaliano ya kumuunga mkono waziri huyo na kufikisha jumla ya wabunge 69 wanaopendekeza Kindiki kuliongoza eneo hilo.