KPLC yatangaza maeneo ya kaunti 9 yatakayokosa umeme leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Septemba 17.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Kiambu, Machakos, Laikipia, Murang'a, Kitui, Mombasa, Kwale, na Tana River.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Septemba 17. 

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Kiambu, Machakos, Laikipia, Murang'a, Kitui, Mombasa, Kwale, na Tana River.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kilimani, Kasarani Icipe, Seasons na Clay City zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Shadenet, Ondiri, na Rorie katika kaunti ya Kiambu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kathome nna Kyumbi katika kaunti ya Machakos yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri.

Maeneo ya Khe na Mukima katika kaunti ya Laikipia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri.

Eneo la Githambo katika kaunti ya Murang'a litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kitui, maeneo ya Migwani na Thokoa yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, eneo la Jomvu katika kaunti ya Mombasa litaathirika.

Maeneo ya Galu katika kaunti za Kwale na Tana River pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.