Wazazi na wanafunzi waandamana kutokana na ukosefu wa usalama - Elgeyo Marakwet

Wazazi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet mashariki walazimika kuwaondoa wanafunzi shuleni baada ya kuhofia upunguzi wa usalama maeneo humo.

Muhtasari

•Wazazi kutaka serikali kuingilia kati hili kutatua swala la ukosefu wa usalamajambo ambalom lilifuatia wazazi hao kuwaondoa wanafunzi wao shuleni kwa hofu ya kushambuliwa.

•Kamanda wa polisi wa Marakwet mashariki Josphat Chacha aliweza kuwahakikishia wakaazi wa eneo hilo kwamba wanafanya juhudi ili kurejesha usalama. 

police car
Image: hisani

Wazazi pamoja na wanafunzi kutoka shule za msingi za Chemisto, Mungwa na Cheptany zilizoko katika eneo bunge la Marakwet mashariki,kaunti ya Elgeyo Marakwet walifanya maandamano kufuatia kile wanachodai ni kuwa upungufu wa shughli za usalama,huku kisa cha hivi majuzi mtu mmoja akiangamia mikononi mwa wahuni.

Baadhi ya wazazi walisema kuwa,wameonelea ni vyema kuwaeka wanafunzi wao nyumbani hadi pale sw3ala la usalama litatatuliwa ,licha ya kuwa ni jamboambalo litakuiwa lisilo na uendelevu hususan kimasomo,maisha ya usoni mwa wanafunzi hao.

Aidha,walisema kuwa licha yakuwa wamepiga hatua na kuripoti lalama zao kwa kitengo husika,hakuna hatua ambayo imeweza kuchukuliwa ,wakisema si mara moja wala mbili.Ni jambo ambalo limewapelekea wazazi hao kufanya maamuzi hayo. 

Kwa sasa wametaka serikali kuingilia kati na kutatua swala hilo ndiposa wanafunzi wakaeze kurejea mashuleni kutamatisha muhula wa tatu.

Mathew Chelimo,mmoja wapo wa mzazi alielezea kuwa,"tumefanya malalamishi kwa mamlaka ya kitengo cha kudumisha amani,na kufikia sasa hakuna hatua imeweza kuchukuliwa,na tuliamua kuwatoa wanafunzi wetu shuleni kwa sababu tunahofia usalama wao kwamba huenda wakashambuliwa"

Patrick Ruto mzazi pia alimuunga mkonoChelimo na kusema wangetaka serikali ifanye kweli na kutafuta suluhu la kutua kwenye maeneo hayo.

Baada ya malalamishi hayo,kamanda wa polisi wa Marakwet mashariki Josphat Chacha aliweza kuwahakikishia wazazi kwamba usalama utaweza kurejea kwenye hali ya kawaida .