Kuna haja ya kudhibiti utayarishaji wa maudhui- MCK

MCK Iliendesha majadiliano wa jopo katika chuo kikuu cha Agha Khan kwa kusudio la kudhibiti kazi za waunda maudhui.

Muhtasari

•Baraza la vyombo vya habari hapa nchini Kenya imeanza mchakato wa kuweka vidhibiti kwa waunda maudhui.

•Omwoyo alitoa wito wa kuanzisha vikwazo vya kuingia ili kuleta ubora kwenye tasnia ya uanahabari.

MCK CEO,KATIKATI
Image: FACEBOOK

Baraza linalosimamia shughuli za vyombo vya habari hapa nchini Kenya, MCK, imesema kwamba ipo haja ya kukumbatia sheria za kiuvumbuzi kutokana na uendelevu wa kiteknolojia hasa akili bandia (AI) kwenye uundaji maudhui.

Mkurugenzi mtendaji katika baraza hilo David Omwoyo alisema kuwa kamati ya kisheria ya wanahabari lazima iweke sheria ambazo zitapiga jeki uadilifu kwenye uanahabari ili kulinda maslahi ya umma na uhuru wa wanahabari.

"Wadhibiti lazima waanzishe miongozo ambayo itakayoweka utofauti kwenye kutofautisha uhuru wa wanahabari,ubora wa wanahabari na kulinda kuingiliwa kwa wanahabari kutokana na vyombo vya nje".

Omwoyo,alizungumza maneno hayo akiwa katika mjadala wa jopo ambao ulikuwa umeandaliwa ukikusudia mada ya kudhibiti vyombo vya kidijitali vya habari katika ukanda wa Afrika, mdahalo huu uliendeshwa katika katika chuo kikuu cha Agha Khan mnamo Septemba 19.

Aidha, aliendelea kutoa wito wa kuanzisha vikwazo vya kuingia ili kuleta ubora kwenye tasnia ya uanahabari, vile vile, alisema kuwa watahakikisha kuwa katika juhudi za kufanisha kanuni za uanahabari ulio bora pindi tu waundaji maudhui wataelewa muingiliano uliopo baina yao na uanahabari.

"Mbinu za udhibitishaji lazima zigusie maswala ibuka na changamoto kuu ambazo zimeibuliwa na uanahabari wa kidijitali hususan kwenye kuunda maudhui.Hii inaweza ikahusisha ushirikiano na washikadau mbali mbali ili kutengeneza mazingira salama ambayo yatawezesha kunawiri kwa uanahabari kwa ujumla".  Alisema.

Wakati uo huo, meneja wa Afrika na mashariki ya kati, hazina ya kimataifa kwa maslahi ya uanahabari Nkirote Koome,alidokeza kuwa mfumo wa kudhibiti kanuni za uundaji maudhui ,zitachangia pakubwa katika hatua ya kukumbatia uvumbuzi ndani na nje ya taifa.

"Kuna haja ya ushirikiano wa kimataifa ili kuoanisha viwango.Hii itajumuisha ushirikiano kwa wadau ikuijumuisha kampuni za kiteknolojia na vikundi asasi za kiraia ili kuweka usawa kwenye mfumo wa kukuza uvumbuzi vile vile kulinda maslahi ya umma".Alisema.